Tuesday, January 26, 2016

CHRIS BROWN APONEA TUNDU LA SINDANO

  Mwanamuziki Chris Brown safari hii amenusurika kukutana na kifungo baada ya polisi wa Las Vegas kuamua kutomfungulia mashtaka kwa kinachoelezewa ni kutokupatikana ushahidi wa kutosha.
   Chris ambae alikua akituhumiwa kumpiga ngumi LIZIANE GUTIERREZ ambae alimtuhumu Chris kumshambulia na kumsababishia maumivu wakiwa kwenye sherehe huko California kwenye ukumbi wa Palms Casino Resort mnamo tarehe 2 mwezi wa huu. 

 
LIZIANE GUTIERREZ
                                                                 CHRIS BROWN

                                                                                 
  Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kupata matatizo kama hayo,ikumbukwe mwaka 2009 alifungwa kifungo cha miaka sita kabla ya kubadilishiwa baadae na kuwa kifungo cha nje baada ya kupatikana na hatia ya kufanyia shambulizi la kumpiga na kumjeruhi vibaya aliekua mpenzi wake RIHANNA.